Friday, December 13, 2013

Wachezaji Yanga waomba kuonana na Manji

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini.
Na Wilbert Molandi
WACHEZAJI wa Yanga wameomba kuonana na mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kumaliza muda wake baada ya kusema hana mpango wa kugombea uongozi klabuni hapo mara baada ya muda wake wa kuwepo madarakani kumalizika.
Yusuf Manji.
Akizungumza, nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema hajajua sababu ya mwenyekiti huyo kutopanga kugombea tena, hivyo kwa niaba ya wenzake ameomba wakutane kwa ajili ya kuzungumza naye masuala kadhaa.
Cannavaro alisema mwenyekiti bado anahitajika katika timu hiyo katika kuleta maendeleo na hasa kipindi hiki ambacho timu hiyo inajiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi kuu Bara pamoja na michuano ya kimataifa mwakani.
“Ujue hadi hivi sasa wachezaji kinachoendelea kuhusiana na Manji kujitoa Yanga hatukijui vizuri, kikubwa tunachokiomba ni kukutana na mwenyekiti. Ninaamini ni kiongozi bora atakayeipa maendeleo na mafanikio timu yetu, ni vema akaendelea kuiongoza Yanga,” alisema Cannavaro.
Straika wa timu hiyo, Jerry Tegete, naye alisema: “Mimi sijui chochote kinachoendelea, kikubwa nasikia amejitoa Yanga, hivyo ni vema tukakutana naye kwa ajili ya kuzungumza naye ili kujua kinachoendelea

No comments:

Post a Comment