Maafisa wawili wa kijeshi wakiwa wamevalia sare nyeupe wamesimama kulinda kila mlango wa kuingilia jengo la ushirika huko mjini Pretoria huku wakiwa na majambia waliyoyaelekeza ardhini.
Mapema maandamano ya mazishi ya Mandela yazunguka kupitia jiji la Pretoria hadi kwa umati wa watu waliokuwa wakisherehekea na kupunga hewani bendera kabla ya kupelekwa ikulu ambako baada ya familia kutoa heshima za mwisho mjukuu wamkubwa wa Mandela aliketi chini tayari kwa kupokea marais, watu mashuhuri na viongozi mbalimbali.
Hapo jana katika ibada maalumu ya kumuombea kiongozi huyo iliyofanyika kwenye uwanja wa FNB mjini Soweto, viongozi mbalimbali duniani walishiriki na kumwelezea Mandela kuwa mtu wa pekee na mfano wa kuigwa.
Kwa upande wa rais wa Marekani Barack Obama amemtaja Mandela kama kielelezo cha jinsi gani watu wanaweza kufikia mabadiliko kwa kupigana kwa ajili ya maadili yao na kujenga hoja na sababu kufikia kujitoa kwao.
Obama amesema kuwa ni vigumu kumsifia mtu yeyote , lakini ni vigumu zaidi kufanya hivyo hasa kwa mkongwe wa historia , ambaye amelifikisha taifa katika haki,na mtu aliyemfanya yeye ashawishike kuingia katika siasa, Nelson Mandela.
Aidha rais Obama amesema kuwa kifo cha Mandela kikumbukwe kwa kipindi cha maombolezo lakini pia kikumbukwe kwa kipindi cha kuhamasisha wakati watu wakitazama jinsi gani wanaweza kubadilisha maisha yao.
Rais Obama amefuatana na marais watatu wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, George W. Bush na Bill Clinton,katika shughuli hiyo maalum.
Mandela anatarajia kuzikwa Jumapili Disemba 15 kijijini kwake Qunu.

No comments:
Post a Comment