Kesi ya Seiful Islam Gaddafi kusikilizwa Febr. 2014
Kesi inayomkabili Seiful Islam Gaddafi mtoto wa Kanali Muammar Gaddafi kiongozi aliyeondolewa madarakani nchini Libya anayekabiliwa na tuhuma za kutenda jinai na mauaji nchini humo imeakhirishwa hadi tarehe 27 Februari mwakani.
Mahakama ya Libya inayofungamana na wanamgambo wa nchi hiyo imetangaza kuwa, mahakama hiyo itaendelea kusikiliza kesi hiyo licha ya kutakiwa kuacha kuendesha kesi hiyo. Seiful Islam Gaddafi anashikiliwa na kundi moja la wanamgambo huko al Zantan tokea ulipoangushwa utawala wa baba yake nchini Libya.
Wanamgambo wa eneo la al Zantan wamekataa kumkabidhi Seiful Islam kwa mahakama ya Tripoli kwa madai kwamba, Mahakama za a Tripoli ziko legelege kiutendaji. Hali kadhalika, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inamtuhumu Seiful Islam Gaddafi kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu nchini humo.
Hivi karibunin Ali Zaidan Waziri Mkuu wa Libya alisema Tripoli haitawakabidhi Seiful Islam na Abdallah as Sanussi mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la nchi hiyo, kwa mahakama ya ICC.
No comments:
Post a Comment