Monday, December 9, 2013

Tanzania bara yaadhimisha miaka 52 tangu kupata uhuru wake toka kwa Waingereza

Gwaride katika maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania bara
http://www.kibonde24.com

Watanzania hii leo wanaadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete anaongoza mamilioni ya wananchi katika kusherehekea kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9 Desemba mwaka 1961, kabla ya Taifa hilo kuungana na Zanzibara mwaka mwaka 1964 na kuzaliwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam chini ya kauli mbiu isemayo “Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu, Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ya Taifa Letu.
Baba wa Taifa la Tanzania Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa sana kwa harakati zake za kuhakikisha Tanganyika inapata uhuru wake toka kwa Waingereza.
Tanzania inafanya maadhimisho haya wakati bendera yake ikipepea nusu mlingoti kufuatia msiba wa kinara wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kiongozi wa kwanza mzalendo nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyefariki dunia tarehe 5 Desemba 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais Kikwete alitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba 2013 na kuagiza bendera zote kupepea nusu mlingoti ili kumuenzi Hayati Mandela.
Vikundi mbalimbali vya utamaduni, gwaride na ngoma za asili vimejiandaa kutumbuiza Watanzania waliofika kuhudhuria sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment