Monday, December 9, 2013

Bunge la Afrika Kusini kumuenzi Mandela wakati watu maarufu duniani wakijiandaa kushiriki kumbukumbu ya kumuaga kiongozi huyo kesho jumanne

Hayati Nelson Mandela
USA Today/capture écran

Bunge la Afrika Kusini linakutana kumuenzi Baba wa Taifa hilo na kinara wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi Hayati Nelson Mandela aliyefariki dunia alhamisi ya juma lililopita nyumbani kwake jijini Johanesburg. Kikao hicho kinakuja wakati viongozi mbalimbali duniani wakijiandaa kushiriki ibada ya kumbukumbu maalumu ya kitaifa hapo kesho jumanne kumuenzi Mzee Mandela.

Watu zaidi ya 80,000 wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya kesho katika uwanja wa FNB mjini Soweto ambao ulitumika katika michuano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2010, Mzee Mandela alifika ulikuwa wa mwisho kushuhudia Mandela akishiriki kwenye shughuli za umma.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama ni miongoni mwa wakuu wa nchi zaidi ya 70 wanaotarajiwa kufika kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Nelson Mandela.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ni mongoni mwa viongozi maarufu wanatarajiwa kuwasili nchini humo.
Usalama umeimarishwa na takribani wanajeshi 11,000 wameandaliwa kuhakikisha hakuna uvunjifu wowote wa amaani unaojitokeza.
Jana jumapili wnaanchi wa Taifa hilo waliungana katika ibada maalumu kumuombea Mzee Mandela, huku Rais Jacob Zuma akiwa katika kanisa la Bryanston jijini Johannesburg aliwataka wananchi wake kutosahau maadili mema walioyoachiwa na kiongozi huyo.
Mwili wa Mandela utalazwa ikulu kwa siku tatu kuanzia jumanne katika majengo ambayo kiongozi huyo aliapishwa kuliongoza Taifa hilo kama Rais wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika mwaka 1994.
Kila asubuhi jeneza lililohifadhiwa mwili wa Mandela litazungushwa katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo ili kutoa nafasi kwa wanachi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mazishi ya mwisho yanayotarajiwa kufanyika jumapili ya tarehe 15 Desemba

No comments:

Post a Comment