MAHARI YA LULU LAKI 8
Imevuja kuwa mwanaume atakayetaka kumuoa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ atalazimika kutoa si chini ya shilingi laki nane (800,000) kama mahari ili kumuoa mwigizaji huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha blog hili, wanaume wengi wamekuwa wakimendea kufunga ndoa na Lulu lakini wakashindwa njia za kumpata.
Ilidaiwa kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia na kigezo cha dini kwa sababu Lulu hataki kuolewa na muislam kwani hayupo tayari kubadili dini.
“Unajua Lulu ameshakua, mambo ya kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya kizamani.
“Siwezi kupanga mahari, sijui laki nane au laki ngapi. Kiasi chochote ni sawa cha msingi mwanangu awe amekubaliana na huyo mwanaume.
Kwa upande wake Lulu alisema: “Kwa sasa sina wazo la kuolewa ila naweza kuamka kesho nikabadili uamuzi.” Alipoulizwa kama ni kweli atatakiwa kulipiwa mahari ya laki nane alisita kidogo.
Kuhusu kigezo cha dini staa huyo alikiri kuwa kati ya vitu anavyozingatia ni hicho kwani hataki mwanaume wa kumbadilisha dini na mahari yake itategemea na mtoaji
No comments:
Post a Comment