Ijumaa, Disemba 13, 2013
Siku kama ya leo miaka 10 iliyopita sawa na tarehe 13 mwezi Disemba mwaka 2003 Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq alitiwa mbaroni akiwa katika maficho yake karibu na Tikrit huko kaskazini mwa Baghdad. Saddam alijificha katika eneo hilo baada ya Iraq kuvamiwa na majeshi ya Marekani na Uingereza mwezi Machi 2003. Kutiwa nguvuni dikteta huyo wa Iraq aliyemwaga damu za raia wengi wa nchi hiyo kuliwafurahisha sana Wairaki na nchi kama vile Iran na Kuwait ambazo zimepatwa na maafa makubwa kutokana na udhalimu za Saddam Hussein dhidi ya nchi hizo. Katika upande mwingine, pamoja na kuwa walimwengu walikuwa wakisubiri kwa hamu kusikia jinai zilizotendwa na dikteta huyo wa zamani wa Iraq wakati wa utawala wake, Marekani ilimweka dikteta huyo chini ya uangalizi wake baada ya kumtia nguvuni lengo likiwa ni kuzuia kufichuliwa ushirikiano wa karibu uliokuwapo kati ya dikteta huyo na serikali za Magharibi khususan ikulu ya Marekani ya White House.
Miaka 88 iliyopita katika siku inayosadifiana na ya leo, Majlisi ya Waasisi nchini Iran ambayo iliundwa kwa ajili ya kuhamisha mfumo wa kisultani kutoka silsila ya Qajar hadi utawala wa kifalme wa Pahlavi, ilitekeleza kazi yake kwa kufanya mabadiliko ya kimsingi katika Katiba ya Iran. Kwa msingi huo utawala wa miaka 153 wa wafalme wa Kiqajari nchini Iran ulifikia kikomo na badala yake ukaanza utawala wa miaka 53 wa Pahlavi hapa nchini.
Na siku kama ya leo miaka 143 iliyopita Ufaransa ilianza oparesheni ya kivita kwa lengo la kuzikalia kwa mabavu ardhi za magharibi mwa Afrika. Oparesheni hiyo iliyodumu kwa miaka kumi ilipelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya wanajeshi na askari polisi wa Ufaransa ambao walikabiliwa na harakati za ukombozi za makabila ya Magharibi mwa Afrika. Hata hivyo kutapakaa huku na kule kwa makabila hayo na kukosekana umoja miongoni mwa tawala za magharibi mwa Afrika na vilevile hatua ya Ufaransa ya kutumia silaha za kisasa kuliiwezesha nchi hiyo kuzikalia kwa mabavu nchi nyingi za Kiafrika zikiwemo Senegal na Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment