Wakati wa Mwalimu, Mawazo na fikra zake ndio yaliyokuwa yanakiongoza chama cha Mapinduzi, wao wenyewe hata wenyeviti wote wa CCM Taifa baada ya Mwalimu walikuwa wanasema zidumu fikra za mwenyekiti, wakati huo wakiwa ni makada wa kawaida wa Chama hicho.

Fikra za Mwalimu hazikukiongoza chama cha Mapinduzi peke yake, ziliongoza Taifa zima katika kila namna, wakati huo kulikuwa hakuna hoja zinazokumbatia rushwa,wizi,ujingaujinga na uchafu mwingi unaonekana katika Chama cha Mapinduzi, serikali na hatimaye Taifa zima kwa sasa.

Angalia Marekani, Fikra za Obama ndio zilizotamalaki katika taifa hilo leo, Marekani ya sasa sio kama ya Bushi na Baba yake, haivamii mataifa ya watu hovyo hovyo, ohoo USA INTERNATIONAL POLICY, mbona policy hiyo hiyo haipigi watu leo?

Angalia Man U, Fergie kaondoka kaingia nani sijui, anajua mwenyewe anavyoendesha timu hiyo akiwa na wachezaje wale wale walio achwa na Fergie.

Mifano ni Mingi, Angalia, Kenyatta alivyobadirisha mahusino ya nchi za Africa Mashariki, Dada Joyce na Ziwa Nyasa n.k

Taasisi ya aina yoyote ile inaendeshwa na watu fulani wachache au hata mmoja, kama a/wana Fikra sahihi uongozi wao utaambana na mafanikio kwa mujibu wa malengo ya taasisi hiyo, kama wanafikra za hovyo a/watafanya mambo ya hovyo.

Uislamu wa leo, chini ya Mashehe hawa, umejaa matatizo hauwezi kuulinganisha na Uislamu wakati wake yeye Mwenye Mtume Mohamed, Ukirsto wa Yesu na wanafunzi wake kumi na mbili unaeleweka ulivyo tofauti na huu wa sasa.

Hata pale tunapofanya mambo ya hovyo, tukiamua kumsingia shetani huwa hatusemi mashetani wamenipitia, tunasema ibilis amenipitia na meli ikizama atakewajibika ni dereva wake, sio yeye na kondacta kwa pamoja.

sasa mtu mzima na akili yake, anaandika tena maelezo marefu kwelikweli kwamba CHADEMA ni zaidi ya Mbowe,DR SLAA,MTEI nakadharka alafu anasema Uongozi wa sasa unakipeleka chama ndivyo sivyo, huwa inamaanisha nini?