Kwanini Mbowe alikuwa anasita Zitto asifukuzwe ndani ya chama?
-

SIRI zimeanza kufichuka!.
Wajumbe wa Kamati Kuu na baadhi ya wanachama wa CHADEMA hawakufahamu kwa nini Mh. Mbowe alikuwa anamkingia kifua Mh. Zitto ili asifukuzwe na hii imeleta msuguano sana ndani ya chama.
Mh. Zitto naye alipokuwa anatamba na kusema 'kunizodoa' mimi ni 'kukizodoa' chama kuna wengine hawakufahamu alikuwa ana maana gani.
Hata tamko lililotolewa juzi la kusema kuwa viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA wasimpe Mh. Zitto nafasi kwa sasa ya kufanya mikutano kwa jina la CHADEMA lilikuwa lina maana ambayo wachache walielewa.
Baadhi ya SIRI NZITO zilizosababisha Mh. Mbowe kusita kufanya maamuzi hayo zimeanza kujitokeza ambazo impliedly zilikuwa zinasababisha Mh. Mbowe kutotaka Mh. Zitto afukuzwe ndani ya chama.
Mh. Mbowe alihofia kufukuzwa kwa Mh. Zitto itakuwa ni kuruhusu kuanikwa kwa siri zake za maisha ya kisiasa na kijamii. Mh. Mbowe alifahamu kuwa kumfukuza Mh. Zitto ni kufungua mlango wa madhambi yao ya kisiasa kuonekana na 'wapita njia' kutokana na ukaribu wao waliokuwa nao miaka mingi.
Kwa sasa tumeanza kufahamu kuwa, viongozi wa CHADEMA ni "double agent", kwa maana kuwa, wanapiga kelele mchana majukwaani kuwa Mh. Nimrod Mkono na Rostam Aziz kuwa ni mafisadi halafu usiku wanakutana na hao 'mafisadi' kupata 'mgao' wao.
Kwa mujibu wa maelezo yao ambayo wanayoendelea kutuhabarisha, 'Mafisadi' wamewanufaisha kwa vitendea kazi vya kwao binafsi na chama ambavyo viliambatana na mamilioni ya shilingi. Kwa lugha nyingine, CHADEMA inaendeshwa na pesa za 'mafisadi'.
Kila siku tuliwambia kuwa CHADEMA ni chama cha kilaghai na kitapeli lakini kuna watu bado walikuwa hawatuelewi.
They are having to live a political lie and they'll die in political lie.
Hawawezi kutumia ulaghai kupambana na ukweli. The chickens have come home to roost.
Kwa faida ya taifa letu endelevu, tunaomba wafukuzane kwa sasa ili tufahamu ukweli wa utapeli wao kisiasa katika taifa letu.
No comments:
Post a Comment