Tuwaombee wenzetu
=============
TAARIFA RASMI:
SMZ imethibitisha boti ya Kilimanjaro2 kupata dhoruba na mpka sasa watu wa tano wamefariki na waliotupwa baharini ni 27 na sasa waliookolewa ni watatu na wamesitisha mpaka kesho usafiri wa majini huko Zanzibar.
Boti hyo inamilikiwa na kampuni ya Azam.
By GHIBUU:
Asalamau Alaykum
Maiti ni wawili wanawake na watatu wanaume kwa mujibu wa taarifa za sasa hivi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Bw. Abdi Omar amesema usiku huu katika taarifa yake na waandishi wa habari huko Bandarini Malindi. Mkurugenzi anasema bado wataendelea kesho asubuhi kuwatafuta wa!tu waliopotea baharini katika maeneo ya Nungwi.
Maiti wote wameletwa mjini kwa ajili ya kutambuliwa wapo katika hospitali ya Mnazi Mmoja baadae serikali itaanda utaratibu wa kawaida kwa maiti hizi kuzikwa kama ni kupewa jamaa zao. Kempteni Nassor Abubakar Khamis ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi anasema baada ya kupata hizo taarifa waliwahoji wahusika wa boti lakini Manahodha wa boti hiyo alisema hajaona kama kuna watu wamepotea lakini wao waliona mizigo tu imeanguka. Mkurugenzi Abdi aliwaambia waandishi wa habari kwamba Manahodha hao walipofika Nungwi kuna watu waliwauliza ikiwa kuna tatizo baada ya kuona boti yao inazunguka zunguka hapo hapo lakini walijibu kwamba hawana tatizo na wanaendelea na safari lakini pia wakaulizwa na KMKM iwapo wanahitaji msaada lakini walikataa na kusema hawana tatizo na wakaendelea na safari.
Mkurugenzi huyo amesema juhudi za serikali zilichukuliwa lakini alikubali kwamba wananchi ndio waliosaidia kwa kushirikiana na vyombo vya usalama kusaidia kuwatafuta waliopotea. Mkurugenzi Abdi anasema kwa kufichwa taarifa hizi kumesbabisha matatizo na kiukweli wangepewa taarifa mapema na Manahodha basi wangeweza kuchukua juhudi za haraka kufanikisha uokozi huo lakini wamepata taarifa kutoka kwa wananchi na sio kwa wahusika wa boti hiyo.
Anasema jumla ya abiria 396 walisafiri na chombo hicho huku watoto wakiwa ni 60 lakini baada ya kufanya hesabu wakakuta idadi hiyo imepunguwa kuna watu kama 20 wamekosekana ndani ya chombo hicho na ndipo walipolazimika kufanya uchunguzi na kufuatilia huko Nungwi na kweli wamepata miili mitano na waliookolewa wakiwa hai ni watatu.
Naomba kuwasilisha
Salma Said.
Bandarini Zanzibar
Reply
Ngambo Ngali 10:52 Yesterday
Pamoja namaombi inabidi rescue services ziwahi, je wana habari
Reply
Gogle 10:54 Yesterday
Meli iko maeneo ya mkondo wa nungwi, hali ni mbaya, wahisika aw uokaoji nendeni kwa haraka
Reply
Tangopori 10:55 Yesterday
Dah! Poleni sana!
Mungu awanusuru ndugu zetu hao!
Reply
Gogle 10:56 Yesterday
By Tangopori:
Dah! Poleni sana!
Mungu awanusuru ndugu zetu hao!
Nashukuru MUNGU tangopori hujaomba picha, MUNGU waokoe ndugu zetu
Reply
CYBEgbRTEQ 10:57 Yesterday
By Tangopori:
Dah! Poleni sana!
Mungu awanusuru ndugu zetu hao!
Seriously?
Reply
Nyamgluu 10:59 Yesterday
Hapo aambiwe bakhresa haraka atatuma rescue team! Ila sijui iambiwe serikali, tutaokota maiti nyingi!
Reply
Tangopori 11:01 Yesterday
By CYBERTEQ:
Seriously?
mkuu CYBERTEQ ebu nisaidie nimekosea nini hapo ili nirekebishe! Maana ninaweza dhani niko sahihi kumbe nimekosea!
Reply
ALLY MALCOM X DEE 11:01 Yesterday
Mungu waokoe waja wako
Reply
life is Short 11:04 Yesterday
Ujumbe umefika Wandugu tuungane mkono na tunyanyue juu kwa maombi ya uhakika. NUSURA NUSRA,Nusura kwa wafamaji NUSRA
No comments:
Post a Comment