Nolesy na Mtafya ni marafiki wawili
walioivana na kupendana sana
tangu wakiwa wadogo mpaka
walipomaliza shule na kuanza kazi
wakiwa pamoja.
Mtafya yeye alifanikiwa kuwa
mfanyabiashara na Nolesy yeye
akabahatika kuwa wakili wa
kujitegemea.
Wote walipata umaarufu katika
kazi zao na wakawa wakikaa
katika nyumba moja ya kupanga
na kila mara baada ya kazi
walionekana pamoja na hata ile
mida ya chakula walikula pamoja
na kisha kurudi makazini mwao.
Mwaka mmoja baadae Mtafya
alifanikiwa kujenga nyumba na
wote wakahamia na kuishi kwa
pamoja.
Nolesy yeye alikuwa na gari na
kwa kuwa hakuwa na safari nyingi
zaidi ikabidi gari liwe linatumiwa
na mtafya ambaye yeye alikuwa na
shughuli mbalimbali za kibiashara.
Maisha yakazidi kuwa mazuri na
wakasaidiana mpaka Nolesy
akajenga na kuhamia katika
nyumba yake na maisha yakawa
mazuri na wakakubaliana
kuendelea kulitumia lile gari kwa
pamoja.
Haikupita muda Nolesy akaamua
kumuoa rafiki yake wa miaka
mingi aitwaye Habiba na harusi
ilifana sana chini ya uenyekiti wa
mtafya.
Maisha yakaufungua ukurasa mpya
na sasa mtafya akawa lazima ale
chakula cha asubuhi, mchana na
jioni pale kwa Nolesy.
Na kwa kuwa gari lilikuwa
likitumika na mtafya alitakiwa
kumpitia asubuhi swahiba wake
kwenda kazini baada ya kupata
chai, mchana wakati wa chakula
na jioni wakitoka kazini na baada
ya mizunguko.
Kama haitoshi mara moja moja
kwa kuwa Nolesy alibanwa na kazi
za kimahakama hivyo mtafya
alimsindikiza shemeji yake Habiba
sokoni kwa ajili ya kutafuta
mahitaji nyumbani na hali ile
ilidumu.
Tetesi zikaanza kuenea mtaani
kuwa Mtafya anatembea kimapenzi
na shemeji yake na habari hizo
zikamfikia Nolesy.
Nolesy hakuwa na pupa
akaendelea kufuatilia mpaka siku
moja saa saba mchana
alipowafumania katika chumba
kimoja cha hoteli iliyojificha
ambako yeye alienda kwa shughuli
za kikazi kabla ya kuwafuma baada
ya kuliona gari lake na begi ya
mkewe ikiwa kwenye siti ya mbele
bila wao na kisha kumwomba
mhudumu ampeleke akidai ana
ahadi nao.
Nolesy baada ya kuwafumania
hakusema kitu zaidi ya
kuwasalimia kisha akarudi mpaka
pale ofisini akamalizana na
mwenyeji wake kisha akarudi zake
nyumbani.
Huku nyuma mtafya na habiba
jasho likawa lawatiririka wasijue
nini cha kufanya.baadae
wakaamua kuondoka zao mpaka
karibu na kwa Nolesy kisha
akamshusha habiba na habiba
kwa upole akaingia nyumbani.
Akamkuta Nolesy akiwa
kashaandaa chakula na kamwekea
maji ya kuoga na kumwomba mke
wake akaoge na akaja wakala na
Nolesy akawa kama kawaida bila
kumuuliza kitu na uchangamfu ule
ule.
Hali ile ilidumu kwa siku kadhaa
kabla ya habiba kukimbilia kijijini
kwao kwa baba na mama yake
ambako hakuongea kitu kwa aibu
na hofu.
Siku chache baadae Nolesy
akamfuata na kumrudisha
nyumbani bila ya kuwaambia
wazee nini kilitokea hata pale
habiba alipolazimishwa aombe
msamaa yeye alisema hajakosewa.
Zikapita wiki kadhaa tangu warudi
mjini na ikawa ni siku nyingi tangu
Mtafya waonane na Nolesy pale
hotel akiwa na mkewe, hivyo
ikambidi Nolesy amwambie habiba
waende kwa mtafya.
Kufika pale wakaona ni kama
nyumba haina mtu kwani gari
lilikopaki ni kama halijaondolewa
kwa siku kadhaa na kuingia ndani
wakamkuta Mtafya akiwa kalala
kwenye sofa na inaonyesha huwa
hatoki zaidi ya kula mikate na
chupa za bia zilizozagaa pale
ndani.
Kuwaona tu akaanza kulia na
kumwomba msamaha Nolesy kwa
kutembea na mke wakati wao
walikuwa marafiki.Nolesy
akasema nimekusamehe na
nilishasahau ila nimemleta huyu
akae akusaidie maana inaonyesha
huwa huli hapa wala kufanya kazi.
Habiba alitaka kukataa lakini
alisalimu amri baada ya Nolesy
kuonyesha hana masiara. Na
kumwambia kuwa kama itatokea
siku naye mtafya akasalitiwa na
habiba kamwe asimdhuru na
kuwa kimya kama yeye Nolesy
alivyowafanyia na kisha
akaondoka.zake na kuwaacha.
Zikapita siku, mara miezi huku
mtafya akiwa anakaa na habiba
kama mke wake na Nolesy
akiendelea na kazi zake za kila siku
akiwa na furaha na kampata
mchumba mpya aitwaye Rehema.
Siku moja Mtafya akawa anasafiri
kutoka pale mjini kwenda kijijini
kuangalia miradi yake. Kufika njiani
akapata tatizo la gari, ikambidi
aliache gari pale na fundi ili yeye
arudi nyumbani kuchukua gari
lingine ili aendelee na safari.
Kufika nyumbani kwake akaona
mlango uko wazi na kuingia moja
kwa moja mpaka chumbani na
kuona habiba akiwa na rafiki yake
aitwaye Salva wanakula tunda la
mtu wa kati kati.
kwa hasira akachukua kisu na
kumchoma Salva na kelele za
habiba zikawaita majirani na kuja
pale kabla ya Mtafya kuchukuliwa
na kupelekwa polisi kwa kesi za
kumuua mgoni wake.
Habari zile zikamfikia Nolesy
ambaye akatumia nguvu na uwezo
wake wa kitaaluma mpaka Mtafya
akaachiwa huru na mahakama
kwa kuua bila kukusudia na kurudi
uraiani baada ya kukaa mahabusu
kwa zaidi ya mwaka na nusu.
Baada ya kutoka mtafya akajiuliza
maswali mengi:
1. Nilitembea na mke wa Nolesy na
kuusaliti urafiki wetu na akaniacha
huru bila kunidhuru.
2. Nikakaa kwa msongamano wa
mawazo akaja na kuniambia
amenisamehe
3. Nimeua baada kumfumania mtu
na mke wangu na bado akajituma
na kunitoa na niko uraiani......
Ananitakia nini mimi
NOLESY?????????
BAADA YA KUTOPATA MAJIBU YA
MASWALI HAYO HATIMAYE MTAFYA
ALIAMUA KUJINYONGA
Tafadhali usisahau ku LIKE Page Hii
No comments:
Post a Comment