Sunday, January 19, 2014

Nolesy na Mtafya ni marafiki wawili
walioivana na kupendana sana
tangu wakiwa wadogo mpaka
walipomaliza shule na kuanza kazi
wakiwa pamoja.
Mtafya yeye alifanikiwa kuwa
mfanyabiashara na Nolesy yeye
akabahatika kuwa wakili wa
kujitegemea.
Wote walipata umaarufu katika
kazi zao na wakawa wakikaa
katika nyumba moja ya kupanga
na kila mara baada ya kazi
walionekana pamoja na hata ile
mida ya chakula walikula pamoja
na kisha kurudi makazini mwao.
Mwaka mmoja baadae Mtafya
alifanikiwa kujenga nyumba na
wote wakahamia na kuishi kwa
pamoja.
Nolesy yeye alikuwa na gari na
kwa kuwa hakuwa na safari nyingi
zaidi ikabidi gari liwe linatumiwa
na mtafya ambaye yeye alikuwa na
shughuli mbalimbali za kibiashara.
Maisha yakazidi kuwa mazuri na
wakasaidiana mpaka Nolesy
akajenga na kuhamia katika
nyumba yake na maisha yakawa
mazuri na wakakubaliana
kuendelea kulitumia lile gari kwa
pamoja.
Haikupita muda Nolesy akaamua
kumuoa rafiki yake wa miaka
mingi aitwaye Habiba na harusi
ilifana sana chini ya uenyekiti wa
mtafya.
Maisha yakaufungua ukurasa mpya
na sasa mtafya akawa lazima ale
chakula cha asubuhi, mchana na
jioni pale kwa Nolesy.
Na kwa kuwa gari lilikuwa
likitumika na mtafya alitakiwa
kumpitia asubuhi swahiba wake
kwenda kazini baada ya kupata
chai, mchana wakati wa chakula
na jioni wakitoka kazini na baada
ya mizunguko.
Kama haitoshi mara moja moja
kwa kuwa Nolesy alibanwa na kazi
za kimahakama hivyo mtafya
alimsindikiza shemeji yake Habiba
sokoni kwa ajili ya kutafuta
mahitaji nyumbani na hali ile
ilidumu.
Tetesi zikaanza kuenea mtaani
kuwa Mtafya anatembea kimapenzi
na shemeji yake na habari hizo
zikamfikia Nolesy.
Nolesy hakuwa na pupa
akaendelea kufuatilia mpaka siku
moja saa saba mchana
alipowafumania katika chumba
kimoja cha hoteli iliyojificha
ambako yeye alienda kwa shughuli
za kikazi kabla ya kuwafuma baada
ya kuliona gari lake na begi ya
mkewe ikiwa kwenye siti ya mbele
bila wao na kisha kumwomba
mhudumu ampeleke akidai ana
ahadi nao.
Nolesy baada ya kuwafumania
hakusema kitu zaidi ya
kuwasalimia kisha akarudi mpaka
pale ofisini akamalizana na
mwenyeji wake kisha akarudi zake
nyumbani.
Huku nyuma mtafya na habiba
jasho likawa lawatiririka wasijue
nini cha kufanya.baadae
wakaamua kuondoka zao mpaka
karibu na kwa Nolesy kisha
akamshusha habiba na habiba
kwa upole akaingia nyumbani.
Akamkuta Nolesy akiwa
kashaandaa chakula na kamwekea
maji ya kuoga na kumwomba mke
wake akaoge na akaja wakala na
Nolesy akawa kama kawaida bila
kumuuliza kitu na uchangamfu ule
ule.
Hali ile ilidumu kwa siku kadhaa
kabla ya habiba kukimbilia kijijini
kwao kwa baba na mama yake
ambako hakuongea kitu kwa aibu
na hofu.
Siku chache baadae Nolesy
akamfuata na kumrudisha
nyumbani bila ya kuwaambia
wazee nini kilitokea hata pale
habiba alipolazimishwa aombe
msamaa yeye alisema hajakosewa.
Zikapita wiki kadhaa tangu warudi
mjini na ikawa ni siku nyingi tangu
Mtafya waonane na Nolesy pale
hotel akiwa na mkewe, hivyo
ikambidi Nolesy amwambie habiba
waende kwa mtafya.
Kufika pale wakaona ni kama
nyumba haina mtu kwani gari
lilikopaki ni kama halijaondolewa
kwa siku kadhaa na kuingia ndani
wakamkuta Mtafya akiwa kalala
kwenye sofa na inaonyesha huwa
hatoki zaidi ya kula mikate na
chupa za bia zilizozagaa pale
ndani.
Kuwaona tu akaanza kulia na
kumwomba msamaha Nolesy kwa
kutembea na mke wakati wao
walikuwa marafiki.Nolesy
akasema nimekusamehe na
nilishasahau ila nimemleta huyu
akae akusaidie maana inaonyesha
huwa huli hapa wala kufanya kazi.
Habiba alitaka kukataa lakini
alisalimu amri baada ya Nolesy
kuonyesha hana masiara. Na
kumwambia kuwa kama itatokea
siku naye mtafya akasalitiwa na
habiba kamwe asimdhuru na
kuwa kimya kama yeye Nolesy
alivyowafanyia na kisha
akaondoka.zake na kuwaacha.
Zikapita siku, mara miezi huku
mtafya akiwa anakaa na habiba
kama mke wake na Nolesy
akiendelea na kazi zake za kila siku
akiwa na furaha na kampata
mchumba mpya aitwaye Rehema.
Siku moja Mtafya akawa anasafiri
kutoka pale mjini kwenda kijijini
kuangalia miradi yake. Kufika njiani
akapata tatizo la gari, ikambidi
aliache gari pale na fundi ili yeye
arudi nyumbani kuchukua gari
lingine ili aendelee na safari.
Kufika nyumbani kwake akaona
mlango uko wazi na kuingia moja
kwa moja mpaka chumbani na
kuona habiba akiwa na rafiki yake
aitwaye Salva wanakula tunda la
mtu wa kati kati.
kwa hasira akachukua kisu na
kumchoma Salva na kelele za
habiba zikawaita majirani na kuja
pale kabla ya Mtafya kuchukuliwa
na kupelekwa polisi kwa kesi za
kumuua mgoni wake.
Habari zile zikamfikia Nolesy
ambaye akatumia nguvu na uwezo
wake wa kitaaluma mpaka Mtafya
akaachiwa huru na mahakama
kwa kuua bila kukusudia na kurudi
uraiani baada ya kukaa mahabusu
kwa zaidi ya mwaka na nusu.
Baada ya kutoka mtafya akajiuliza
maswali mengi:
1. Nilitembea na mke wa Nolesy na
kuusaliti urafiki wetu na akaniacha
huru bila kunidhuru.
2. Nikakaa kwa msongamano wa
mawazo akaja na kuniambia
amenisamehe
3. Nimeua baada kumfumania mtu
na mke wangu na bado akajituma
na kunitoa na niko uraiani......
Ananitakia nini mimi
NOLESY?????????
BAADA YA KUTOPATA MAJIBU YA
MASWALI HAYO HATIMAYE MTAFYA
ALIAMUA KUJINYONGA
Tafadhali usisahau ku LIKE Page Hii

Saturday, January 18, 2014

LOWASA AANZA KUHUJUMIWA

MKAKATI wa Edward Lowassa kutaka kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huenda ukakwama baada ya baadhi ya vigogo ndani ya chama hicho kupanga mkakati wa kutaka kumfukuza, imefahamika.

Taarifa za ndani ya CCM zinasema mpango wa kutaka kumfukuza Lowassa kutoka chama chake unatokana na hofu ya baadhi ya wagombea wenzake wanaohaha kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015.

Vyanzo vya habari zetu vimemnukuu mmoja wa vigogo waandamizi ndani ya chama hicho akisema, mkakati wa kumvua Lowassa uanachama unasukwa kwa ustadi mkubwa na kigogo mmoja mwandamizi mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali.

“Huyu bwana tayari ameanza mikutano ya kampeni, hata kabla ya chama chetu kutoa mwongozo. Anazunguka nchi mzima kusaka urais. Huku ni kuvunja taratibu. Tutakutana na kumdhibiti,” ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Taarifa zinasema mkakati wa kumfukuza Lowassa utaegemea hoja kuu mbili:

Kwanza, ni madai kuwa Lowassa ameanza kampeni kabla ya chama chake kutoa mwogozo; kujenga mtandao wa ushindi na kudaiwa kupanga safu za uongozi; jambo ambalo linaweza kukidhoofisha chama chake.

Kuhusu tuhuma za kuanza kampeni mapema, mtoa taarifa anasema, Lowassa anatuhumiwa, pamoja na mambo mengine, kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano na baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wenyeviti wa mikoa na makada wengine wa ngazi za kati na kuwashawishi kumuunga mkono katika mbio zake za kusaka urais.

Hata hivyo, mkakati wa kumfukuza Lowassa kwa madai ya kuanza kampeni mapema waweza kukwama kwa kuwa mmoja wa wagombea anayepigiwa chapuo na walioko madarakani, naye tayari ameanza kampeni.

Pili, mkakati wa kumfukuza Lowassa, unatajwa kujikita kwenye madai ya kuhusika kwenye ufisadi wa mkataba tata wa kufua umeme wa kampuni ya Richmond Development Company (RDC).

Wakati mkabata huo unafungwa, Lowassa alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri. Alitajwa na Kamati Teule ya Bunge, kwamba ndiye aliyeshinikiza watendaji serikalini kuipa kampuni hiyo kazi ya kufua umeme. Ilithibitika baadaye kuwa kampuni haikuwa na uwezo, ujuzi wala sifa ya kufanya kazi iliyopewa.

Mtoa taarifa anasema, ni mara baada ya mkutano ambapo taarifa zake zilivuja kwenye chama na serikalini na mpango wa kumfukuza ukafufuliwa upya.

mwandishi wetu alipowasiliana na kiongozi mmoja mstaafu serikalini kuhusu kufukuzwa kwa Lowassa na iwapo mkakati huo unaweza kufanikiwa, haraka alisema, “Hata mimi nimesikia. Nami nimewauliza kama ambavyo unaniuliza wewe, kwamba ‘mtaweza?’”

Anasema amewaambia kuwa huyu bwana (Lowassa) tayari amejijenga ndani ya chama na kwamba hatua yoyote ya kumfukuza sasa inaweza kukivuruga zaidi chama hicho.

Akiongea kwa hasira kigogo huyo alisema, “Huyu bwana (Edward Lowassa), anataka kutuharibia chama chetu. Lazima tumfukuze. Tutaitisha vikao vya Kamati Kuu (CC) na NEC kumjadili. Tunataka tulifanye hili kabla ya mambo kuharibika zaidi.”

Hata hivyo, wapinzani wa mkakati wa kumfukuza Lowassa wanasema, kufanikiwa kwa mpango huo kutakigharimu mno CCM kuliko kumuacha Lowassa hadi mwisho akapigiwa kura na kukataliwa na wajumbe wa vikao vya vyama, mtoa taarifa anasema, Lowassa alitangazia wafuasi wake kuwa ameanza mbio za kutafuta urais; aliahidi kupambana hadi mwisho.

Kuibuka kwa taarifa hizi za kutaka kumdhibiti Lowassa kwa tuhuma za kuanza kampeni kabla ya muda, kumekuja wiki tatu baada ya gazeti hili kuanika orodha ya watu 14 wanaotajwa kutaka kuwania urais, miongoni mwao wakiwa wale wanaodaiwa kuwa tayari wameanza kampeni.

Miongoni mwa wanaotajwa kuanza kampeni, ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Steven Wassira na aliyepata kuwa waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Katika mbio hizo, Membe anatajwa kuunganisha nguvu na Migiro kwa upande mmoja na Samwel Sitta kwa upande mwingine.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, muungano kati ya Membe na Sitta unasukumwa na agenda ya kukabiliana na nguvu ya Lowassa.

“Hata muungano kati ya Membe na Migiro, nao ni kama muungano kati ya Membe na Sitta. Yote hii, inasukumwa na kukabiliana na Lowassa. Sasa ikitokea Lowassa akakatwa mapema, nao hawa wataanza kukimbiana, kila mmoja akitafuta urais kivyake. Maana wataona yule anayewanyima usingizi tayari atakuwa ameshaondoka,” ameeleza mtoa taarifa wetu.

Anasema, “Hata hawa, kama alivyo Lowassa, tayari wameanza kampeni. Mwishoni mwa mwezi uliopita, Membe alikuwa Iringa, ambako pamoja na mambo mengine alikutana na makundi mbalimbali ya watu na kutangaza kugombea urais,” ameeleza kigogo mmoja wa chama hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini

Friday, January 17, 2014

HII IMETOKA JAMII FORUM KAMA ILIVYO

KAULI TATA AMBAZO ZINAZUA MASWALI MENGI KUTOKA KWA MH:FREEMAN AIKAEL MBOWE NI HIZI

1. Kupitia gazeti la majira la wiki tatzu zilizopita Mh.Freeman mbowe alinukuliwa akisema Yupo tayari kuachana na chadema wakati wowote atakapo amua.Kauli hii ni tata na mlengo wake unazua maswali mwengi sana.
Tujiulize mbowe anasema kuwa anatakuacha na siasa za CHADEMA wakati wotete Je ni kwamba amechoka kupigana na CCM?Au ameshavuna mazao ya siasa na hahitaji tena kuendelea kuyala?
Naweza kwenda mbali kabisa kwamba Mbowe anapotangaza kuachana na siasa za CHADEMA ni kwamba anataka kuudhihirishia umma kuwa CHADEMA si mali yake(familia) kama wengi wanavyokitafsili?
Lakini kauli kama hii mbowe haoni kama anakatisha tamaa kwa viajana ambao wamekuwa wakijiunga na CHADEMA kutokana na yeye kuwa mwanaharakati makini kwa muda mrefu?

2. Kupitia GAZETI LA TANZANIA DAIMA wiki iliyopita Mh.Mbowe alitangaza kumkaribisha waziri mkuu wa zamani Mh.Fredrick sumaye kwenye ulimwengu wa siasa za CHADEMA.Swala hili hakika linazua maswali mengi sana.Ikumbukwe SUMAYE ni mmoja ya mafisadi papa wa nchi hii na alikuwemo kwenye LIST OF SHAME iliyosomwa na CHADEMA pale mwembe yanga.Je sumaye ameshakuwa msafi kiasi kwamba anapewa nafasi na CHADEMA?

Kelele za chadema siku zote ni kupingana na rushwa iweje leo mtuhumiwa mkubwa wa rushwa nchini kama sumaye aonekane muhimu mbele ya chadema na hatimaye kumtaka asajiliwe?
Lakini tuende mbali zaidi yawezekana MBOWE anamuita SUMAYE aje chadema kwa ile kauli ya WANYUMBANI NJOO NIKUSHIKE MKONO SIPO RADHI UFIE JANGWANI hatakama ni haramu??????.........ni siku chache sana SUMAYE amebwagwa kwenye uongozi ndani ya ccm na ameishia kulalama kuhusu kufanyiwa mchezo mchafu.

3. Kauli ya tatu tata zaidi ni ile aliyoitoa pale HAI alipokuwa anamkaribisha na kumshukuru Mh.Rais kikwete kwa utendaji wake.Mbowe alinukuliwa akisema"nimetembea angani na aridhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE."
Nachelea kusema maneno hayahaya yangesemwa na chama chochote kingine yangezua gumzo,au yange semwa na mwanachadema yeyote yule yangezua mjadala mkubwa wakitaifa.Naomba kuuliza hii ni kauli sahihi ya kiongozi wa upinzani kumwambia Rais wa nchi hata kama ana show appriciation ya kile kilichofanyika?
Hakuna lugha nyingine yakipinzani-yakusifia ambayoingetumika hapa???Mbowe huu ni wakati wakuwekana wazi kwa watanzania, KAMA UKOMBOZI UMESHAUZWA NI HERI WATANZANIA WAKAAMBIWA kuliko maneno kama haya ya kusifia kupitiliza as if nchi hii hakuna upinzani.WANA-JF nawasilisha naomba tujadiliane kwa makini namna kauli hizi zinavyoathiri chama na zinavyojenga chama.

UNAAMBIWA HUYU MTANGAZAJI ANAMILIKI JUMBA KALI ZAIDI LA HUKO MAREKANI, TAZAMA PICHA HAPA


Ellen DeGeneres ndio wanasema mtangazaji anayeishi kwenye jumba kali zaidi huko L.A Marekani. TMZ wame ripoti kuwa jumba hili ni kali na lenye thamani kubwa zaidi kuliko jumba lake la awali alilonunua. 


Jumba lake la sasa lina thamani ya dola milioni $39,888,000 na linaitwa The Brody House. Kiwanja kina eka 2.3 , vyumba sita vya kulala, mabafu sita, bwawa la kuogelea , sehemu ya mazoezi na uwanja wa kucheza tennis.


SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

JE WADADA WA MJINI MNAWEZA TOKELEZEA NA HII VAZIIII??? NIJUZE


SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

HAKUNA KAMA DIAMOND TANZANIA, HII NDO GARI YAKE MPYAAAAAAAAA. INAUZWA ZAIDI YA MILIONI 100 ZA KIBONGO ICHEKI HAPA

 Hahaaaa kweli diamond noma sana, wanaosema ana hela kibao hawajakosea kabisa kwani kwa mafanikio aliyonayo na anaendelea kupata sidhani kama atafilisika leo. Najua kuna wengi mnaweza bisha na kusema kwani Mr Nice alikua wapi na leo yupo wapi, but ukweli ni kwamba Diamond na Mr Nice wanautofauti mkubwa katika kupanga na matumizi ya mshiko.

Hii si siri tena kua kwa sasa Diamond ndo anaongoza kwa kua msanii anaelipwa mshiko mrefu kuliko wote hapa bongo na nahisi anaelekea kua hata Afrika Mashariki. Nina ushahidi kidogo tu kua admin wenu wa Bongoclan nilipokua likizo katika jiji la Mwanza Diamond alipiga show katika jengo la Buzuruga Plaza na kulipwa shilingi Milioni 23. Sidhani kama kuna msanii yoyote wa bongo alishawahi kulipwa mshiko huo kwa show moja, ili afikishe mshiko huo nahisilazma apige kuanzia show 3 hadi 4 ili amfikie Damond.

Tuache Brabra na tuende kwenye utamu wenyewe, kama mnakumbuka miezi michache iliyopita msanii Diamond alinunua gari aina ya Toyota Prado na ilikua gumzo sana mtandaoni na kwenye magazeti ya udaku. Sasa baada ya mshiko kuongezeka kaamua kununua gari ambayo ni funiko yani hakuna msanii mwenye kiburi wala jeuri ya kununua gari hiyo. Maana akijaribu tu basi ujue uchumi wake utatetereka mbaya, nayo si nyingine ni Toyota Land Criser V8 Mpyaaaaaaaaaaaaaa.

Katika fukunyuafukunyua ya timu yetu  tukagundua kua ili mtu aweze nunua gari hiyo ni lazima awe na dola za kimarekani 70,000 au ambayo ni zaidi ya milioni 110. Hakika ni gari ya ukweli sana na hapa bongo wanaotumia magari haya kwa wingi ni watu wenye vyeo vikubwa serikalini mfano JK, Pinda na baadhi ya mawaziri.


SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

RIHANA NOMA SANA ANASWA AKIOGELEA MTONI BILA AIBU, NI HUKO BRAZIL. TAZAMA PICHA HAPA



SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

KAMPENI ZA UDIWANI MBUNGE WA CHADEMA AJIKUTA AKIJIHUTUBIA MWENYEWE NA WASHIKAJI ZAKE ALIOENDA NAO ONA NOMA HII LIVE!!



Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni za chadema kata ya Nduli, Iringa, leo

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba leo wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema


Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano huo












Na Francis Godwin Blog
IKIWA ni siku mbili toka katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Hassan Mtenga kumwagiza mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kufuatilia kero mbili za wananchi ikiwemo ya wagonjwa kukosa dawa katika Hospital ya mkoa na kujua fedha za ruzuku ya jimbo la Iringa mjini ziko wapi na zinafanya nini, mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna kiasi cha Tsh milioni 30 nyingine za mfuko wa jimbo.

Huku mbunge Msigwa akiwaomba radhi wananchi wachache waliofika katika mkutano huo kwa kudai kuwa haukutangazwa vya kutosha .

Hatua ya katibu huyo kuagiza kufuatilia fedha hizo ni baada ya jimbo hilo kukabiliwa na changamoto mbali mbali na fedha hizo zinazotolewa na Rais zimelenga kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini Manispaa ya Iringa fedha zinakaa bila kazi.

Akizungumza katika mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli leo ,Msigwa alisema kiasi hicho cha Tsh 30m zipo hadi sasa.

“Naomba kuwahakikishieni nitaendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kusaidia kero za maji hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe Ayub Mwenda nitafanya nae kazi”

Pia Mbunge Msigwa amesema kuwa katibu wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake ila yeye saizi yake ni akina waziri mkuu Mizengo Pinda,waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani Wiliam Lukuvi na katibu mkuu wa CCM Bw Kinana na sio yeye .

“Nataka kuwahakikishia kuwa huyu mimi si saizi yangu saizi yake ni akina Frank Nyalusi diwani wa Mvinjeni (Chadema) na katibu mwenzake wa Chadema Iringa mjini Suazana Mgonakulima.

Wao wanasema amekuja kwa ajili ya kunishughulikia mimi ila nasema njia aliyojia atatitoka na njia hiyo hiyo kama walikuwepo akina Charles Charles na wametoka zaidi ya makatibu 7 iwe yeye .

Hata hivyo katika mkutano huo ambao idadi ya watu ilionekana ni ndogo zaidi ukilinganisha na hali halisi ya nguvu ya Chadema iliyokuwepo jimbo la Iringa mjini ,bado mbunge huyo alitumia mkutano huo kuwaomba radhi wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi kwa madai haukutangazwa vya kutosha.

Kampeni za uchaguzi mdogo wa kata hiyo ya Nduli zimeanza rasmi leo kwa Chadema kufungua pazia hilo huku wao CCM wanataraji kuzindua kampeni hizo katika eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu

Uchaguzi huo mdogo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Idd Rashid Chonanga aliyefariki duni kwa ugonjwa mapema mwaka jana.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa Chadema katika kata hiyo ya Nduli Ayub Mwenda ambae alipata kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Nduli kabla ya CCM kumsimamisha nafasi hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za maendeleo ,alisema kuwa yeye ana risiti za fedha zote ambazo alikuwa akikusanya na kuwa kusimamishwa kwake nafasi ya uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Lusiana Mbosa na kuwaomba wananchi kumkubali sasa ili awe diwani wa kata hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Iringa wanadai kuwa kipimo cha kukubalika ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo hilo kwa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi za serikali za mitaa ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli

SOURCE BONGO CLAN

AADA YA MAINDA KUTANGAZA KUOKOKA NA KUMRUDIA MUNGU, HUYU NDO MSANII MWINGINE WA BONGO MOVIE ALIYETANGAZA KUOKOKA


Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’.
WASANII wa filamu, Ruth Suka ‘Mainda’ na Salome Ndumbagwe Mesayo ‘Thea’ sasa wameonekana kujikita zaidi kwenye mafunzo ya kiroho baada ya hivi karibuni kunaswa kwenye kongamano la ukombozi ndani ya Ukumbi wa Vatican City Sinza jijini Dar walipokwenda kuabudu.
Ruth Suka ‘Mainda’.
Wawili hao walinaswa wakiwa na nyuso za unyenyekevu huku wakionekana kudhamiria kumrudia Mungu na walipoulizwa walisema walikuwa katika kongamano hilo la mafunzo ya kiroho na Biblia kwa siku tatu.
 
 “Sisi tumempokea Yesu, tunawasihi wasanii wenzetu waachane na ushirikina waje huku ambako kuna njia salama, hili ni kongamano ambalo lina mafunzo mema na lina uwezo wa kumbadili mtu kutoka kwenye roho ya kishetani na kuwa na roho safi,” alisema Thea....
CREDIT : GPL

source bongo clan

DUNIA IMEISHA, SASA KANYE WEST KUANZISHA DINI YAKE. HAYA NDO MAAJABU YA DINI HIYO. SOMA HAPA



Attention! Dini mpya kabisa duniani inaitwa Yeezianity .  Jina hili linafanana na album mpya ya kanye inayoitwa Yeezus ambayo ni combination ya  nickname yake ya Ye na jina la  Jesus. Tayari kuna website kwa ajili ya waumini inayoitwa Yeezanity.com . Wafuasi wa dini hiyo wanatumia sanamu linalofanana kabisa na uso wa Kanye West. Founder wa dini hii alisema ““Kanye West is the most honest person in our culture.He has the highest moral standards and highest integrity. He is the most creative person. And as it’s typical with creative people, he gets a lot of flack from the lower minded masses. It’s not even that they don’t like him, it’s that they don’t know what he’s doing because the press gives it this negative spin all the time”
yeezus
Ukitaka kujiunga na dini hiini rahisi sana.Unachotakiwa kufanya ni kuwatumia email yenye picha isiyokutambulisha ukiwa umeshika karatasi lililoandikwa ‘I Believe In Yeezus’.


Tuesday, January 14, 2014

'Niliula mguu wa adui kulipiza kisasi' 

Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda kati ya jamii za waisilamu na wakristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, BBC imegundua mambo ya kutisha yanayofanyika mjini Bangui, mji mkuu wa taifa hilo.
Wanaoyashuhudia baadhi ya mambo hayo wameambia BBC kuhusu kisa cha mwanamume mmoja anayejulikana kwa jina la utani kama "Mad Dog," kuwa alimkata mguu muisilamu mmoja baada ya kumuua akisaidiwa na umati wa watu na kuula.

Aidha mwanamume huyo kwa jina Ouandja Magloire alisema kuwa kila mtu ameghadbishwa na wapiganaji waisilamu na hakuna atakayewasamehe kwa walichokifanya.Mwanamume aliyekifanya kitendo hicho ameambia BBC kuwa alifanya hivyo kama hatua ya kulipiza kisasi baada ya wapiganaji wa kiisilam kumuua mkewe aliyekuwa mja mzito na wifi yake pamoja na mwanawe.
Anasema alimuona mwathiriwa akiwa ameketi ndani ya basi moja. Alimtoa nje na kuanza kumshambulia na punde si punde akasaidiwa na umati uliokuwa unashuhudia kitendo hicho ambao pia ulimshambulia mwathiriwa huyo.

"Muisilamu! Muisilamu! Muisilamu!. Nilimdunga kisu kichwani na kummwagia petroli kisha kumteketeza. Baadaye nikaanza kuula mguu wake mmoja kwa Mkate hadi kwenye mfupa. Ndio maana watu wananiita Mad-dog," alisema Magloire.

'Nilifanya hivyo kwa sababu nina uchungu mwingi, wala sina sababu nyingine.''
Hali ilivyo kwa sasa katika taifa hilo hakuna hata mtu mmoja aliyejaribu kumnusuru mwathiriwa. Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na ghasia za kidini tangu Machi mwaka 2013 ambapo wapiganaji wa kiisilamu walimsaidia aliyekuwa Rais Michel Djotodia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi.
Kisa hiki hata hivyo kimewashangaza wengi sana . Na hali hii ikijiri, Mamia ya wanajeshi wa serikali walioasi jeshi na kujiunga na wapiganaji wakristo katika vita vyao dhidi ya waisilamu,wameanza kurejea katika kambi zao za kijeshi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wanajeshi hao wengi wao wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia walitia saini makubaliano na wakuu wa jeshi kabla ya kurejea kambini. Ni kutokana na ombi la mkuu wa majeshi Ferdinand Bomboyeke, aliyewasihi kurejea kambini Jumatatu

Monday, January 13, 2014

 Huyu ndiye muigizaji brian deacon aliyeigiza kama "yesu" na anachokifanya kwa sasa katika maisha..!!


Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi. Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.


Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu. 
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa. 
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu. 
kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia j


SOURCE: JAMII FORUMS 

Wednesday, January 8, 2014

Wanaosema chadema sio mbowe , slaa, ex naibu k.mkuu, mtei n.k wanamaanisha nini?.

Wakati wa Mwalimu, Mawazo na fikra zake ndio yaliyokuwa yanakiongoza chama cha Mapinduzi, wao wenyewe hata wenyeviti wote wa CCM Taifa baada ya Mwalimu walikuwa wanasema zidumu fikra za mwenyekiti, wakati huo wakiwa ni makada wa kawaida wa Chama hicho.

Fikra za Mwalimu hazikukiongoza chama cha Mapinduzi peke yake, ziliongoza Taifa zima katika kila namna, wakati huo kulikuwa hakuna hoja zinazokumbatia rushwa,wizi,ujingaujinga na uchafu mwingi unaonekana katika Chama cha Mapinduzi, serikali na hatimaye Taifa zima kwa sasa.

Angalia Marekani, Fikra za Obama ndio zilizotamalaki katika taifa hilo leo, Marekani ya sasa sio kama ya Bushi na Baba yake, haivamii mataifa ya watu hovyo hovyo, ohoo USA INTERNATIONAL POLICY, mbona policy hiyo hiyo haipigi watu leo?

Angalia Man U, Fergie kaondoka kaingia nani sijui, anajua mwenyewe anavyoendesha timu hiyo akiwa na wachezaje wale wale walio achwa na Fergie.

Mifano ni Mingi, Angalia, Kenyatta alivyobadirisha mahusino ya nchi za Africa Mashariki, Dada Joyce na Ziwa Nyasa n.k

Taasisi ya aina yoyote ile inaendeshwa na watu fulani wachache au hata mmoja, kama a/wana Fikra sahihi uongozi wao utaambana na mafanikio kwa mujibu wa malengo ya taasisi hiyo, kama wanafikra za hovyo a/watafanya mambo ya hovyo.

Uislamu wa leo, chini ya Mashehe hawa, umejaa matatizo hauwezi kuulinganisha na Uislamu wakati wake yeye Mwenye Mtume Mohamed, Ukirsto wa Yesu na wanafunzi wake kumi na mbili unaeleweka ulivyo tofauti na huu wa sasa.

Hata pale tunapofanya mambo ya hovyo, tukiamua kumsingia shetani huwa hatusemi mashetani wamenipitia, tunasema ibilis amenipitia na meli ikizama atakewajibika ni dereva wake, sio yeye na kondacta kwa pamoja.

sasa mtu mzima na akili yake, anaandika tena maelezo marefu kwelikweli kwamba CHADEMA ni zaidi ya Mbowe,DR SLAA,MTEI nakadharka alafu anasema Uongozi wa sasa unakipeleka chama ndivyo sivyo, huwa inamaanisha nini?
 

By; Albert Msando,Kupitia ukarasa wake wa Fb haya ndio aliyoandika. 

Kwa marafiki zangu,

Hatujashinda kesi dhidi ya chama. Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA.

Natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA mojawapo ya madhumuni ya chama ni kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi ....

Pia natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya chama Wajibu wa mwanachama wa Chadema ni kuwa tayari kupambana na namna yeyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi.

Wajibu huu ni ndani na nje ya chama. Hatuwezi kutekeleza wajibu upande mmoja. Binafsi ninalo jukumu kutekeleza wajibu wangu kwa manufaa ya chama.

Kumekuwa na lawama, shutuma na malalamiko kwamba nilichokifanya kinadhoofisha chama. Napinga kwa nguvu zangu zote. Inawezekana kabisa nilichofanya kinadhoofisha watu wachache ndani ya chama ila sio CHAMA. 

CHADEMA sio mtu binafsi. Ni taasisi. Wanachama wake ndio nguzo muhimu. Sio Zitto wala Mbowe wala Slaa. Hawa ni viongozi tu ambao wajibu wao ni kuendelea kujenga chama.

Uwezo wao upimwe kwa matokeo ya sasa. Sio kwa mvuto na haiba zao. Fundisho la haya yote ni moja: KUVUMILIANA SIO KUFICHIANA SIRI AU UDHAIFU. Kosa limetendeka na kukubali kosa sio dhambi. 

Ni wazi kabisa kumekuwa na kutokuelewana kwa muda mrefu. Ni dhahiri viongozi wetu wamekuwa wanajua udhaifu wa kila mmoja wao. Lakini kwa sababu ambazo hazijawa wazi waliamua kukaa kimya. Au labda ilikuwa ni kwa kuamini kwamba yatamalizika bila athari. Sasa matokeo yake ndio haya.

Kinachohitajika sasa sio kutafuta mchawi. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha suluhu inapatikana. Na niseme wazi kabisa, kama suluhu ni mtu kufukuzwa basi tuhakikishe hilo linafanyika kwa mujibu wa Katiba na Kanuni kwa kuzingatia haki za msingi kama ambavyo tumekuwa tukipigania. 

Haki itendeke, na zaidi lazima ionekane imetendeka. Pamoja tunaweza. 

Mwisho, tusiruhusu muendelezo wa 'ufuasi' wa watu ndani ya chama. Tuwe wafuasi wa misingi ya chama. Bado nafasi ipo ya kurekebisha pale tulipoangukia kama busara na hekima vitatumika.

Nawatakia kila kheri ndugu zangu. 

"In a battle for the minority rights we have to promote the rights of the majority and we will remain united" AGM 2014.

Msando

TUNDU LISU akiwa Mahakamani pamoja na ZITTO KABWE

TUESDAY, JANUARY 07, 2014
MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAAMURU CHADEMA KUTOJADILI UANACHAMA WA ZITTO KABWE MPAKA KESI YAKE YA MSINGI ITAKAPOSIKILIZWA TENA



Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.

Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.


Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.


Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.



Tundu Lisu akiwatuliza na kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.

 Watanzania Wanajiaandaa Kukikabithi CHADEMA Dola.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya chadema, Profesa Mwesiga Baregu, amesema viongozi wa chama hicho wanapaswa kulinda kauli zao ili kuepuka mvuragano unaoweza kutokea wakati huu.

Wakati huu ambao chama kimekuwa na mambo mengi, nawasihi viongozi kuchunga kauli zao ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza.

“Nimekuwa msuluhishi ndani ya chama, nakwambia ndani ya chama haiwezekani fikra moja ikaendelea kudumu, kwa msingi huo lazima watu watofautiane mtazamo, si kila jambo kupinga.

“Katika hali hii, msimamo wangu ni kwamba changamoto inayotukabili tupunguze makali ya maamuzi, kwa sababu Watanzania wengi wanakitegemea chama hiki.

“Hivi sasa Watanzania wanajiandaa kukikabidhi CHADEMA dola,
 ni wakati mzuri wa viongozi kufikiria maisha ya chama kwanza na baadaye ukweli wa mambo utajulikana,” amesema.


zitto kabwe


Yafuatayo ni maswali na majibu aliyoyatoa Zitto.
millardayo.com : Unadhani utakua na amani kuwa Chadema pamoja na haya yaliyotokea?
Zitto kabwe: ‘Kwanza nataka niseme wazi kabisa kwa Watanzania ambao ni Wanachama wa vyama vingine, wasio na vyama na kwa Wanachadema, ushindi huu sio ushindi dhidi ya Chadema, ni ushindi kwa Watanzania wote wanaopenda siasa safi, wanapenda taratibu za utawala bora zifatwe kwenye taasisi zetu, ni ushindi dhidi ya wanaotaka kukandamiza demokrasia ndani ya vyama, ni ushindi dhidi ya Wahafidhina wasiotaka mabadiliko katika vyama’
Huu sio ushindi dhidi ya chama kwa sababu siwezi kushindana na chama changu, ni chama ambacho kimenilea na nimekitumikia kwa muda wangu wote, zaidi ya nusu ya umri wangu ambao nimeishi…. kwa hiyo salamu ambazo napenda wananchi wazifahamu ni kwamba tunahitaji kuheshimu sana demokrasia na misingi ya haki za binadamu.
Naamini maamuzi ya Jaji John Utamwa yataweza kuweka utaratibu, watu ambao ni Wanachama wa vyama hawataonewa, hawatadhulumiwa wala kukandamizwa, watakua huru kutoa maoni yao pale wanapohitaji kufanya hivyo.
millardayo.com : Kilichotokea Mahakamani kitakufanya usiende kwenye ofisi za Chadema?
Zitto Kabwe: Hapana kwa sababu bado mimi ni Mwanachama wa CHADEMA, pamoja na kwamba katibu mkuu wa Chadema ametoa amri ya watu wasinipe ushirikiano lakini pale nitakapohitajika nitafanya shughuli za Chadema, nitafanya shughuli za nchi yangu.
Sasa hivi kuna maswala makubwa kuhusu katiba ya nchi yetu na ningependa Wananchi wajielekeze huko, sijafurahishwa sana na kinachoendelea hivi sasa manake Wananchi wameacha kujadili maswala ya msingi sana ambayo yanawahusu, nasikitika kuona vyombo vya habari ni habari za Zitto na Chadema, nashukuru jambo hili limekwisha sasa kwa muda huu.
Mimi niko tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote wa CHADEMA ambae atakua tayari kufanya kazi na mimi kwa sababu naamini swala hapa ni ujenzi wa nchi yetu, ni ujenzi wa taifa letu na ninaamini hata kama nina mawazo kidogo lakini ninayo mawazo kwa ajili ya kuiendeleza nchi yetu.