Ningependa kuuliza , hivi kweli Tanzania kuna wasomi? Na kama wapo je ni viashiria (indicators) gani vya kuonesha kuwa hii nchi ina wasomi tena wengi?
Naomba msinishangae kwakuwa aulizaye ataka kujua jamani, na kwakuwa nijuavyo mimi ni kwamba msomi ni yule anayetumia elimu yake kufanya vitu vinavyoonekana, haogopi kufukuzwa kazi kwa kutimiza wajibu wake kitaaluma, ni mkereketwa wa kweli wa nchi na rasirimali zake, hawezi kukwepa wajibu wake hasa pale wajibu huo unapoangukia kwenye eneo husika na alichosomea na ni muumini mzuri wa miiko ya taaluma yake.
Tanzania ya sasa ina professors wangapi? Ina PhD holder’s wangapi? Ms wangapi?
Muonekano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii unahakisi idadi ya wasomi tulio nao nchini?
Tanzania ya enzi za wasomi wachache na ya sasa ni sawa?
Kama ni kinyume na muonekano bora, je tunaweza kujua ni kwanini tuna non performer scholastics nchini?
Nawasilisha wakuu.
Tuesday, February 25, 2014
Wasomi na hatima ya tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment