Najaribu kufikiri sanaaaaaa
TUNAKUMISS SANA J.K.NYERERE
1. Idd Amini - Alipoivamia Tz....Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda.......
2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo...Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..
3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi pale UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli "Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.." Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...
4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere
akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..
5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!..Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...
6. Edward Lowassa-Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!..Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!..
Wakamuuliza Nelson Mandela,tukupe nini ili uache usumbufu na harakati zako,wakampa cheki ajiandikie kiasi cha fedha,yeye akaigeuza kwa nyuma akaandika UHURU NA USAWA WA WATU WANGU-
Hakuna tena mfano wa viongozi hawa siku hizi.
Wednesday, February 26, 2014
Najaribu kufikiri sana: TUNAKUMISS SANA J. K. NYERERE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment