Universal secrets......!!
Habari zenu wapendwa,
kuna hiki kitu kinaitwa universal secrets, yaani siri za ulimwengu au siri za dunia hii tunayoiishi. Kawaida mtu unazaliwa na unaanza kupata kumbukumbu at least kuanzia miaka miwili na nusu au mitatu ila tangu ukiwa umezaliwa hadi kufika miaka mitatu hata umeditate vipi huwezi kukumbuka zaidi yake utahadithiwa kuwa ulikuwa mlizi sana, ulikuwa hupendi watu, ulikuwa unapenda kula, ulikuwa mjanja na uliwevuka haraka kuliko umri n.k
Kilichonifanya nifikirie kuhusu hizi universal secrets ni kuwa pale hasa kutoka miaka 0 hadi 3 kama watu wangekuwa wanazaliwa wanaongea wangetoa siri za universal maana ile lugha hakuna anayeweza kuijua na ndio maana watu husema watoto wachanga ni malaika.
Mfano mawasiliano ya mtoto na mama huwa ni ya kuguess kuwa mtoto huyu akilia anataka nini au kwa nini leo halali hana usingizi kabisaa au leo kalala sana. Iwapo watoto hawa wangeweza kusema wangetoa siri nyingi za dunia na ulimwengu huu.
Kilichonisukuma hasa kuandika uzi huu ni baada ya kusoma ule uzi wa kusoma saa kinyume na mshale unavoelekeza, hadi naingia mitamboni hakuna aliyekuja na jibu sahihi, wengine wakasema ni free masons and the like ila to me ni universal secrets. Na mwanadamu anapotafuta kujua universal secrets ndo hapo mtu anaenda beyond thinking yaani anakuwa yuko ulimwengu mwingine na anapokuja na data kujaribu kuzishare na dunia hakuna anayemuelewa na wengine wanamuona chizi.
Hii ni pamoja na wanaokuja na stori za kusema walishawahi kufa na kufufuka na muda wamekufa vitu walivyoona wakivisimulia huku duniani huwa wanadhihakiwa kuwa hawakufa bali walizimia na hivo wanavosimulia wanaambiwa ni ndoto tuu au maluweluwe yamewapanda kichwani na watakuwa wanasumbuliwa na malaria.
Sasa basi naomba wanajamvi wote wenye interest na hii universal secrets kuchangia chochote unachojua kuhusu siri za dunia hii japo wapo wanaosema ukifanikiwa kuzijua siri za ulimwengu huu huwezi kuishi utakufa tuu.
Ushawahi kusikia watu wakisema watoto wachanga huwa waanaona wachawi?
Kuna wanyama pia wanashirikishwa kwenye siri hizi za ulimwengu kama mbwa na paka, je unalolote zaidi ya haya ambayo ungependa kutushirikisha, karibu kuchangia.
No comments:
Post a Comment