Thursday, March 20, 2014

SIMULIZI "RAFIKI WA MAWANAMKE"


"Leo lazima nikuvunje miguu yote miwili mchawi mkubwa wewe" Ilikuwa ni sauti yenye hasira kali ikisikika, huku sauti ya mwanamke aliyekuwa anaongea kwa unyonge na kuomba msaada ikisema "Jamani unaniua mume wangu. Mama nakufa nisaidieni jamani nakufa" Jirani kulikuwa na wakinamama wameketi huku wakisemeshana "Yaani huyo mwanamke ni mjinga sana inamaana kupigwa kote huko bado anaendelea kuishi na huyo bwana" Dada mmoja akaongeza neno "Yaani hata mimi namshangaa sana huyu Mwanadodo, kwanza muache apigwe hadi atolewe macho, mimi wala sijali anayataka mwenyewe, kila siku tunaamua ugomvi tunamwambia aondoke huyu mwanaume hamfai, atakuja kumuua lakini mwenzetu hakomi, hata kama ni mapenzi mimi siwezi unaweza kufa hivihivi unajiona".

 Mmoja kati ya wale kidada aliyekuwa anaitwa Subira alisimama nakusema "Lakini jamani pamoja na yote twendeni tukamsaidie mwenzetu" Wote walimcheka na kunyanyuka huku wakiondoka na kumuacha Subira akielekea katika kile chumba alichokuwa akisikia sauti ya Mwanadodo Aligonga mlango bila ya mafanikio, akiwa ameendelea kusimama pale mlango ulifunguliwa na mume wake Mwanadodo alitoka bila ya kuzungumza chochote na kubamiza mlango kisha kuondoka na kumuacha Subira akiwa ameduwaa.

 SIMULIZI HII INAKUJIA HIVI KARIBUNI USIKOSE KUISOMA HADI MWISHO WAKE.

UKATILI HUU KWA WATOTO HADI LINI "MTOTO ABAKWA KISHA KUVUNJWA SHINGO"



Mtoto wa miaka 13 amekufa wilayani Tarime baada ya kubakwa na kisha kuvunjwa shingo na mtu anayedaiwa kuwa ndugu yake. Mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Nyangoto kata ya Matongo Nyamongo, alifanyiwa unyama huo juzi mchana katika kijiji cha Nyangoto. Mtuhumiwa Nyamatese Mkoma, licha ya  kudaiwa kumvunja shingo pia inadaiwa alimvunja paja la kulia kabla ya kumsababishia kifo. Polisi inamsaka mtuhumiwa. 

Kamanda wa Polisi wa Tarime Rorya, Justus Kamugisha amesema Mkoma alionekana mara ya mwisho akiwa ameongozana na mwanafunzi huyo na baadaye mwili wa mtoto ulikutwa vichakani. Kwa mujibu wa Kamanda, inadaiwa mtoto huyo alivunjwa viungo vyake kwa kile kinachosadikiwa kulikuweko na purukushani wakati akipambana kujiokoa. Mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya unyama huo. Tunamsaka mtuhumiwa huyo. Naomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi letu la Polisi ili tumkamate afikishwe katika mkono wa sheria. Alisema Kamanda. CHANZO HABARI LEO.

SIMULIZI FUPI "YALAITI NINGESIKILIZA USHAURI WA WAZAZI"


Bosco Baada ya kufanikiwa kupata kazi, Alifurahi sana kwani ni muda mrefu alisota mtaani huku akitafuta kazi. Maisha yalibadilika na sasa aliweza kujikimu katika mambo mbalimbali. Katika safari yake ya maisha kabla ya kufanikiwa kupata kazi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mmoja anayeitwa Jeni na walibahatika kupata mtoto mmoja. 

Baada ya mwaka mmoja tokea Bosco aanze kufanya kazi Maisha yake yalikuwa mazuri zaidi na sasa alifanikiwa kununua gari na kuishi katika nyumba nzuri. Ilifikia kipindi wazazi wa Bosco waliamu kumshauri kijana wao aowe. Na mama yake Bosco siku zote alikuwa akimshauri afunge pingu za maisha na jeni ambaye ni mama wa mtoto wake. Jeni yeye alikuwa akifanya kazi ya dukani, kwani hakufanikiwa kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha tano.


 Bosco alikuwa hana wazo la kumuoa Jeni kwani siku zote alikuwa akiwaambia wazazi wake "Kuzaa mtoto na mwanamke siyo lazima kuwa nitamuoa yeye, mimi sina mpango huo nitamlea mtoto wangu lakini suala la kumuoa Mama yake halipo kabisa katika kichwa changu" Alisema Bosco huku Mama yake akiwa anamsikiliza kwa umakini akasema "Lakini mwanangu hapo ulipo umefikia umri wa kuoa na tena, Mungu amekujalia una kazi nzuri sasa sijui kwanini hutaki kuoa, na tena Jeni ni mwanamke mrembo, mpole na mwenye heshima, halafu wewe ndiyo ulimuharibia maisha yake baada ya kumpa mimba akiwa anasoma, leo hii humtaki?"

 Bosco alimtizama Mama yake na kusema "Mama, mimi siwezi kumuoa Jeni, Kwanza nina mchumba wangu ambaye nina mpango wa kufunga naye ndoa" Mama yake alinyamaza kimya na hata Baba yake alipojaribu kumshawishi  alikataa na kuondoka.

Baada ya miezi miwili kupita Bosco aliamua kumleta mchumba wake na kumtambulisha kwa wazazi wake, mwanamke huyu alikuwa anaitwa Tina ambaye alikuwa amemaliza elimu yake chuo kikuu cha Dar es salaam na sasa alikuwa katika harakati za kutafuta kazi. Wazazi wake walikubali kwa shingo upande kwani walikuwa hajaridhika na maamuzi ya mtoto wao. Na kwa upande wa Jeni alisikitika sana kwani siku zote alikuwa akiamini ipo siku atakuja kuolewa na Bosco. 

 Maisha yaliendelea wakiwa jijini Dar es salaam baada ya kufunga ndoa, Bosco alihamishwa kikazi, na kuhamia jijini Mwanza. Wakiwa huko mke wake aliendelea kuhangaika kutafuta kazi bila mafanikio. Bosco aliamua kumshauri Tina afanye biashara, wazo ambalo Tina alilikubali na Bosco alimpa mtaji mkubwa wa kuanza biashara. Alifungua Duka la vipodozi na sasa ilimpelekea kuanza kusafiri kwaajili ya kuja kununua mizigo ya dukani jijini Dar es salaam na wakati mwingine alikuwa akienda China. Siku zilivyozidi kwenda Biashara ilikuwa na hatimaye Tina alikuwa  mfanyabiashara mkubwa wa duka la vipodozi jijini Mwanza. 

Maisha yalikuwa mazuri, Baada ya miezi michache Bosco alipata matatizo katika sehemu aliyokuwa anafanya kazi na kupelekea kusimamishwa kazi. Hivyo alikuwa nyumbani huku akihangaika kutafuta kazi sehemu nyingine. Kama unavyojua kutafuta kazi si lele Mama unaweza ukasota sana. Siku moja Bosco aliamua kuzungumza na mke wake ili waweze kushirikiana katika biashara. Mke wake alimsikiliza kwa umakini na kusema "Unajua unanishangaza sana Bosco, yaani mimi na wewe tufanye biashara pamoja, haiwezekani wewe endelea kutafuta kazi mimi nibaki na biashara zangu, kwani hazikuhusu hata kidogo yaani ni za kwangu peke yangu".

 Bosco alibaki ameduwaa huku akifikiri labda mke wake alikuwa anatania "Embu acha utani mke wangu, mimi na wewe ni kitu kimoja, changu chako, na chako changu, na isitoshe mimi ndiye niliyekupa mtaji hadi biashara imesimama vizuri" Kwa dharau Tina alicheka na kusema "Hahahaha hivi huoni hata aibu, eti nilikupa mtaji, sikiliza nikuambia hapa ndani usipotafuta kazi hauna chako, na kuhusu biashara yangu usiingilie hata kidogo".

 Alinyanyuka na kuondoka huku akimuacha mume wake akiwa ameduwaa, Maisha yalikuwa magumu sana kwa upande wa Bosco kwani mke wake alikuwa hamsaidii kwa chochote ilifikia kipindi alikuwa anasafiri bila hata ya kumjulisha kuwa anakwenda wapi. Baadaye Tina alijigundua kuwa ni mjamzito, Bosco alifurahi sana kwani ijapokuwa na kero zote alizokuwa akizipata kutoka kwa mke wake  lakini siku zote alikuwa akimpenda sana, miezi ilisogea na hatimaye alijifungua salama mtoto wa kiume. 

Maisha yaliendelea huku Bosco akiwa anaishi kwa kumtegemea mke wake. Na kwa kipindi chote alikuwa akivumilia vituko vyote alivyokuwa anafanyiwa na mke wake. Siku moja Tina alikuwa ametoka na kwenda kazini huku akimuacha Bosco akiwa na mtoto nyumbani. Kwa bahati mbaya alisahau simu yake ya mkononi, Bosco aliiona na kuichukua, akiwa anataka kuiweka kwenye droo ghafla ujumbe ulitumwa, jina la aliyetuma lilikuwa limeandikwa (my darling) mpenzi wangu, alishangaa kuona jina hili na kuamua kuusoma ule ujumbe ambao ulikuwa umeandikwa "Mpenzi nimekukumbuka sana, sasa leo naomba uje na mtoto, halafu nachukia sana kuona mtoto wangu analelewa na mwanaume mwingine, fanya mpango umfukuze huyo mjinga wako hapo vinginevyo nitakuja kumchukua mtoto wangu".

 Bosco alibaki akiwa anashangaa asiamini macho yake kile alichokuwa anakisoma, hasira zilimjaa na kuketi huku akiwaza "Inamaana huyu mtoto siyo wangu? Hivi Tina anaweza kunifanyia mimi hivi, inaniuma sana, na leo akirudi, ama zake ama zangu" Baadaye Tina alirudi haraka baada ya kugundua kuwa amesahau simu alipofika alimkuta Bosco ameishikilia simu na kusema "Nani kakuambia unifichie simu yangu, nipe simu yangu, sijui likoje" Bosco alikuwa amekasirika sana bila kuzungumza chochote alimnasa kibao Tina na kusema "Leo utanieleza huyu mwanaume aliyekutumia ujumbe ni nani, na huyu mtoto ni wa kwangu au laa" Tina alimtizama Bosco kwa dharau na kusema "Yaani wewe unanipiga mimi, sasa sikiliza huyu mtoto siyo wako na huyo aliyetuma ujumbe ndiyo Baba yake, na imekuwa vizuri umelifahamu hilo naomba uondoke hapa kwangu kwanza mimi ndiyo ninayetoa matumizi na kulipa kodi ya nyumba, kwahiyo fungasha virago vyako urudi kwenu".

 Bosco aliishiwa nguvu na kujikuta machozi yakimbubujika katika paji la uso wake alitamani kumrukia Tina na kumpiga lakini alijizuia kwa kutuliza hasira zake. Siku hiyo hiyo alikusanya kila kitu chake na kuondoka huku akisikitika sana "Yalaiti ningewasikiliza wazazi wangu leo hii yasingenikuta, ni bora nirudi nyumbani nikaombe msamaha" Kesho yake alirudi Dar es salaam kwa wazazi wake ambao walisikitika sana kutokana na hali aliyokuwa anayo, walimsamehe, na Baba yake alimpa mtaji wa kufungua biashara huku akimtaka asahau yote yaliyotokea. Baada ya muda walionana na Jeni na Bosco alimuomba msamaha na hatimaye baadaye maisha yaliendelea kuwa mazuri na sasa Bosco aliamua kumuoa Jeni na waliishi maisha ya furaha pamoja na mtoto wao. 

Friday, March 14, 2014

Topic: Muda mfupi Kabla ya Kukata roho: NINI HUTOKEA?

Heshima mbele!!

Sijui niseme nimebahatika,au nina bahati mbaya,ya kushuhudia watu watano kwa nyakati tofauti wakikata roho.
Huu ndio uzoefu wangu:
1: Babu yangu alikata kauli kama siku nne hivi.
Siku ya tano akapata faham,tukaongea naye,na alikuwa mchangamfu mno,akituasa sana kuishi vema.
Baadaye akasema ana usingizi.
Akajifunika shuka.
DOKTA alipo kuja dk. Kumi baadaye akatuambia tutoke nje,
punde akatuambia babu ametutoka.
2: Ndugu yangu mwingne.
Alilazwa kwa siku tatu.
Akasisitiza sana mwanae aitwe.
Mwanae alipo fika tu,akamkumbatia,
alipo lala,kesho yake tukaambiwa kafariki.
3: nimewah lazwa hosp,na kuna ndugu alikata roho pembeni ya kitanda changu.
Alihangaika sana kwa kurusha miguu,kujitingsha etc kabla ya kukata roho.
Haya ni ambayo nimeshuhudia.
Lakini kuna tales nyng zingne walizo ona wengine.
SWALI:
Nini hasa hutokea kwenye mind ya mtu kabla ya kukata roho&anapo karibia kukata roho?
Karibuni.


By Pasco:
Hii ni situation inaitwa "near death experience!" ambayo hutokea kabla ya kifo, wakati ambao roho inaacha mwili!.
Nitawahadithia kidogo experience yang na kuwapa za wengine!.
Niliwahi kupata ajali mbaya sana ya pikipiki, ikasemekana "nimekufa!", nikafunikwa kanga, na kuachwa wakisubiriwa polisi kufika kuuchukua mwili!. Kwa kawaida nikikumbuka huwa napata "stigmata" hivyo subirini nipate kidogo, ndipo nije nihadithie, ilikuwaje hatimaye nikawa hai tena1, na mpaka leo mimi nipo!.

.
By hippocratessocrates:
Sijui kama nitakujibu au nitakuwa nje ya mada/swali.
"Kukata roho"..ni neno/msemo tunaoutumia kila leo pale mtu anapokuwa anakuwa/ameacha kupumua na hapa ni zaidi ya kupumua, moyo kutofanya kazi, na viungo vingine vya mwili vikiwepo mapafu, ubongo n.k
Hii ni tofauti kidogo na ile watu wanapoita yuko katika 'Coma/Brain dead'.
Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutegemea msukumo wa damu, hii ikiwa kupitia damu hewa safi na chafu husambazwa mwilini na hata viungo vingi mf. misuli kutegemea nguvu(sukari) kupitia damu hii hii.
Kimabadiliko ya mwili, mtu anapokaribia kukata roho vitu hivi hutokea.
Kupungua kwa shinikizo/msukumo wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hapa namaanisha upungufu wa lishe, hewa safi, na uongezekaji wa taka mwili ambazo zingepaswa kusafishwa.Hii hupelekea
1. 'Kuchanganyikiwa'
Ubongo unapokosa hewa safi, hufanya mtu kuona/kusikia(HASA KUONA) vitu tofauti na wengine. hapa utasikia watu wakisema "eee, marehemu alisema kabisa malaika amekuja kumuijia", au " alituaga kabisa kuwa anaenda mbinguni" n.k
2.Mwili kuwa wa baridi:
Msukumo mdogo wa damu husababishwa upungufu/uwezo mdogo wa mwili katika utoaji wa taka mwili, lakini zaidi hata urudishwaji wa damu ili isafishwe huwa mdogo zaidi.
3. Mwili kutoka jasho, kuhangaika:
Wakati kukiwa na uwiano mdogo wa hewa safi na msukumo wa damu, Bado mwili hujitahidi kutengeneza/kufanya njia za kutafuta uwiano huo kuwa sawa! Hapa mtu atahangaika kuwa kama 'hewa haitoshi', na wakati fulani kutokana na msukumo kidogo ambapo kupitia damu nguvu(sukari hupatikana), mwili hutengeneza sukari(nguvu) mbadala pia kupitia misuli, ambayo kupitia kwayo, jasho pia hutengenezwa/kuzalishwa.
5. Kujisaidia/Kupata haja:
Wakati mwili pia ukiendelea "kuhangaika" kupata nguvu/nishati, baadhi ya 'sphincters' kutegemea nguvu hii au kwa ajiki ya kujikakamua, hasa katika kibofu cha mkojo na mwishoni mwa mfumo wa chakula, hujikuta vikipitisha choo kikubwa/kidogo au vyote.
Haya ni baadhi tu ya MENGI yanayotokea wakati mtu anapokaribia "kukata roho"


By Pasco:
Nimerudi naomba nianze kama ifuatavyo
Kuzaliwa na kifo ni sehemu mbili muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu, kuzaliwa ikiwa ndio mwanzo wa maisha na kufa ndio mwisho wa maisha, kama ilivyo kanuni ya kila lenye mwanzo lina mwisho, hivyo hakuna chochote cha kustusha au kustaajabisha kuhusu kifo kwa sababu tangu ile siku ya kwanza binadamu anazaliwa, ni hakika anajua siku ya siku itafika na atakufa!.
Binadamu ana sehemu kuu mbili, mwili na roho ambayo ndio huo uhai. Kwa mfumo wa imani, mwili umeumbwa kwa udongo, hivyo tumetoka mavumbini, na ni mavumbini tutarudi!. Baada ya kuumbwa kwa udongo, Mungu akatupulizia pumzi ya uzima, huu ndio uhai, hii ndio roho, hivyo mtu anapokufa, kinachokufa ni mwili tuu, roho haifi, bali roho huuacha mwili!, (inakwenda wapi- tembelea Life after death: What Happens After Death? - Jamii Forums). Kitendo cha roho kuuacha mwili, ndicho hicho kiitwacho, kukata roho!, na huo ndio mwisho wa uhai wa mwili, hiyo roho ikiisha uacha mwili, huendelea na maisha mengine, mbinguni, motoni, peponi, ahera, jehanum, kwenye reicarnation, spiritual world, etc!.
Hili la Mwili na Roho, "physical body" na "spiritual body" nimelieleza kwa kirefu katika mada yangu hii Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila Wao Kujijua...nimesema hivi
Kuna aina nyingi za roho kuacha mwili, usingizini, kwa uzee, kwa kuugua, kwa kuuliwa, kwa kujiua au kwa ajali. Hivyo pilika pilika za roho kuacha mwili mara nyingi zinategemeana unakufaje, umejiandaaje kufa, na umejaaliwa kiasi gani kufa kifo chema!.
Kwa wanaokufa kwa kuuliwa, au ajali, mara nyingi hutegemea injury iliyosababisha kifo huanzia wapi, ikianzia kwenye brain au kwenye moyo, then kifo ni instant, there and then!, bila maumivu yoyote na bila kukura kakara zozote, na ndio maana wadunguaji, hulenga kichwa au moyo, na utekelezaji wa hukumu za kifo za kisasa au mtu atapigwa risasi ya moyo, au atachomwa sindano ya sumu kuusimamisha ubongo!, no pain!. Kunyongwa ni unyama!.
Kwa vifo vya uzee, mara nyingi hutokea usingizini, na hawa wazee huwa wamejiandaa kufa, na kuna wengine kutoka na kuzeeka sana, wanamuomba Mungu, awachukue tuu wasiendelee kuwa mzigo kwa waliobaki, hivyo wengi huita watoto wao, huwapa usia, na kusubiria tuu siku ya siku na hawa hawana kutapatapa kwa sababu wame accept death!. Ukiona anaekufa kwa uzee anatapatapa, ujue huyo ama haja accept, au anateseka kufidia mambo fulani mabaya aliyoyafanya wakati wa uhai wake hivyo malipo ni duniani, kama hajafa hupata mateso kufidia, na mateso hayo ndioko kule kutapatapa huwezi jua endaikawa anakula bakora ila nyinyi hamzioni!. "Ila pia kuna wazee ambao wamekataa kukiruhusu kifo, bado wanaishi ila ni katika miili mingine na mahali pengine!"
Wanaokufa kwa ugonjwa nao ni kama wanaokufa kwa uzee, wale wanaoaccept kifo, hufa kimya kimya usingizini, wale wasiokubali matokeo hutaka kulazimisha kuishi, ila ugonjwa tuu wenyewe as ugonjwa ni mapigo, hivyo akitapatapa ujue anamalizia kufidia, hizo pia ni bakora!.
Kwa wanaokufa kwa kuuwawa, au kwa ajali, hawa wanakuwa hawajajiandaa kufa!, hivyo kifo kwao ni unexpected, mtu anaweza kuwa amekufa mwili, ila roho yake bado haijaenda mbali na mwili, hivyo anaona na kuyasikia yote yanayoendelea, sometimes hadi mwili unaposhushwa kaburini, ndipo roho huondoka!. Kwa vifo vingi vya ajali ambavyo miili haikupatikana kufanyiwa mazishi rasmi, baadhi ya roho hizo hubaki zikitangatanga na ndizo mizimu, ama huwatokea watu etc, zinaitwa Ghosts auWandering Spirits, unaweza kunisoma hapa kuhusu hawa "wondering spirits! hapa!, "Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza.
Kisa changu. Mimi ni" bike lover" siku zote usafiri wangu ni bike, ninazo pikipiki 6!, tano kati yake ni big bikes over 750cc!, Mbili nimenunua bongo, tatu niliziagiza, moja niliifuata!. My last bike ni big flying machine aina Harley Davidson "Buel" Firebolt 1200 CC niliinunua US, bongo ilikuwa the one and only na mpaka leo sijabahatika kuona hiyo kitu kwenye streets za bongo, hivyo huwa ninakwenda nayo popote, I simply fly!. Speed yake ni 240kph!.
Wakati maonyesho ya 88 yakifanyika Morogoro, mimi nilikuwa nalala Dar, asubuhi na paa zangu kwenye Moro ni 1:45 hour ride! na jioni narudi Dar!. Dar -Dodoma ni 3:45 hours ride. Dar-Moshi ni 4 hour ride, Dar-Arusha 5hrs ride!, I was simply mad!. Mind well, my wife and my bog boys wote wana drive magari yao, to me bike was my choice for convenience!, hivyo I don't regret what happened to me na bike ilichonifanya!. Na nimefanya safari za hivyo mara kibao!.
Nimeisha onya mara kibao, hatari za kusafiri na bike long distance, sikusikia!. Ukipenda mno bike, unakuwa kama kichaa fulani hivi, husikii mpaka yakukute!. Siku moja nikitoka Dar-Dodoma, nikiwa mwendo wa 160kmh, nilipata ajali mbaya, nikabingirishwa nilipoangukia, ikawa ndio hapo hapo!. Sikujitambua tena mwili, bali nilisikia tuu sauti za watu wakisema, huyu jamaa ameishakufaa hapa hapa!. Nakasikia watu wakisema leta kanga tumfunike, tungojee polisi waje kuuchukua mwili!. From then, sikujua tena nini kilichoendelea!.
Kumbe huku nyuma kuna dereva mmoja wa TAMISEMI naye ni bike love, alikuwa akiipenda sana bike yangu na mara kibao tunapishana Dar-Dodoma. Sasa alipoona ile bike, akaijua na kuuliza huyu jama yuko wapi, akaambiwa kafa pale pale!, akapelekwa kuonyeshwa mwili ulipofunikwa!. Kwanza aliipiga picha ile bike kwa simu yake, kisha akaupiga picha mwili wangu ukiwa umefunikwa. Kisha akasema huyu mwenye piki piki, namfahamu, naomba kumfunua kujiridhisha kama ndiye yeye!, akaifunua ile kanga, kuniangalia akakuta ndiye!, akawauliza umepita muda gani, maana hata damu ilishaanza kuganda, wakamwambia nusu saa!. Akanigeuza kunipiga search akakuta simu, akapiga home na kuwaeleza alichoelezwa!. Sasa katika huko kunigeuza ndipo akasema mbona mwili bado wa moto?!, akanisikilizia kwa karibu akasikia napumua kwa mbali!.
Akasimamia nikabebwa kuwahishwa Dodoma hospital, kwenye pochi wakakuta kadi yangu ya AAR, wakawapigia, mimi kuja kuzinduka ni saa 6 za usiku, nimezungukwa, wife ndugu, waandishi wa Dodoma, polisi, ndipo nikakumbuka kilichotokea na zile sauti za mfunikeni!.
Tangu niliposikia zile sauti za mfunikeni, kimoyo moyo nikajisemea I can't die!. No way!. Kumbukumbu zikapotea mpaka nilipozindukia hospital!. Ndipo nikaambiwa baada tuu ya ajali, walikimbilia kuniokoa, wakakuta sipumui wala sitingishiki, hivyo wakajua nimekufa!.Jamaa akanionyesha zile picha!.
Japo kifo ni kweli kimeumbwa, ukijiandaa na kukubali kufa, unakufa!. Ukisema no to death, no matter umeumia kiasi gani, you might live!. Dodoma wakashauri wafanye amputation ya baadhi ya viungo!, AAR wakazuia, kesho yake asubuhi nikaletewa charter na kuwa flown to Muhimbili, bima yangu ilikuwa ndogo, ingekuwa kubwa ningepelekwa Nairobi. Pale Muhimbili, wakajitahidi walivyoweza, nikapelekwa South huko bili ikawa too much to bear, nikahamishiwa India, japo sikupona kabisa, but I'm still alive!.
Naombeni msiniulize maswali yoyote kuhusiana na hii ajali, ninapata tatizo liitwalo "stigmata" hivyo kurudiwa na maumivu makali!, ila mimi ni miongoni mwa hao tuliopitia "near death experience!".
Asanteni.


Reply
By Apolinary:
Swali lako gumu kulijibu.
Labda waliowahi kukata roho kama wangekua wanarudi kutuambia nini kilitokea. lakini katika hali ya kawaida huwezi kujua ni nini kinatokea pindi Binadam anapouacha Uhai!
Mkuu Apolonary,ni gumu,ila naamini linajibika.
Tuna magwiji wa philosophy,medicine na religious experts humu.
Tusubiri tuone.

Reply
Labda ujaribu kwanza then unaweza kutupatia jibu zuri maada watafiti jufanya majaribio
\
Reply

Mmh maswali mengine bwana, sijui mlengwa ni nani hasa....kuna maswali marahisi ambayo majibu yake ni magumu kama ni nini kinatokea muda mfupi kabla ya kuzaliwa na magumu ambayo majibu yake ni magumu pia kama hili lako la sasa!
Reply
King'asti
Hili Ni suali la msingi Sana. Huwa najiuliza Sana kuhusu hili.
Reply
Money Stunna
Ilo swali gumu kuna mjomba wangu mwaka juzi alituita caracas venezuela hakatuaga na kutoa wosia .
Usiku huo hakafariki ninachoshangaa mbona wengine wanajua siku yao
Reply
Sista
jamani mbonamnatutisha? wengine tuna roho nyepesi
Reply
Bujibuji
Hebu tufanye umwiliisho (reinarnation) Reincarnation - Wikipedia, the free encyclopedia
Reply
kinyoba 18:35 19th February 2014
Naskia roho inapokutoka lazima kimba kidogo kikutoke.. Waswahili wanakuambia inaitwa NGAMA. Yaani cha mwisho kabisa! Ndio maana hata lugha za mtaani utasikia neno NGAMA.. Yaani cha mwisho kabisa alichobakiwa nacho!
Reply
Pasco
Hii ni situation inaitwa "near death experience!" ambayo hutokea kabla ya kifo, wakati ambao roho inaacha mwili!.
Nitawahadithia kidogo experience yang na kuwapa za wengine!.
Niliwahi kupata ajali mbaya sana ya pikipiki, ikasemekana "nimekufa!", nikafunikwa kanga, na kuachwa wakisubiriwa polisi kufika kuuchukua mwili!. Kwa kawaida nikikumbuka huwa napata "stigmata" hivyo subirini nipate kidogo, ndipo nije nihadithie, ilikuwaje hatimaye nikawa hai tena1, na mpaka leo mimi nipo!.
Pasco.
Reply
Myakubanga
By Pasco:
Hii ni situation inaitwa "near death experience!" ambayo hutokea kabla ya kifo, wakati ambao roho inaacha mwili!.
Nitawahadithia kidogo experience yang na kuwapa za wengine!.
Niliwahi kupata ajali mbaya sana ya pikipiki, ikasemekana "nimekufa!", nikafunikwa kanga, na kuachwa wakisubiriwa polisi kufika kuuchukua mwili!. Kwa kawaida nikikumbuka huwa napata "stigmata" hivyo subirini nipate kidogo, ndipo nije nihadithie, ilikuwaje hatimaye nikawa hai tena1, na mpaka leo mimi nipo!.
Pasco.
Rudi mkuu Pasco
Reply
Mtokambali
Nafikiri hata kwa wale tuliowahi kufanyiwa operesheni ukiwekewa ile dawa wanaita nusu kaputi unahama ulimwengu huu,ule si usingizi bali nusu ya kifo. Kwa kawaida mambo unayoongea wakati ukipotelea usingizini na yale utakayoongea au kufanya ukiwa unarudiwa fahamu huwa ni sawa na experience ya mtu anayekufa aise. Na muda wote wa huo usingizi mzito huwa ni kama kifo japo unapumua,ubongo wako unakuwa umeonja mauti....
Reply
Sista
mada nzito hiiii
Reply
bunited
we c ajabu ushaanza kuitwa kwa mungu.fanya mpango anza kugawa urithi.km mjomba wako alipewa cku 4 we umepewa 6.fanya tu uende kwa amani.au muulize mzee wa upako yule anae fufua watu halafu uwaulize wale waliofufuliwa kwamba inakuwaje huko wakuu.
Reply
Myakubanga
By Bujibuji:
Hebu tufanye umwiliisho (reinarnation) Reincarnation - Wikipedia, the free encyclopedia
Ahsante mkuu Bujibuji.
Sasa,ndio kusema pale wanakuwa wanaenda huko kwenye state ya unyama,spirip au ubinadamu mwingine?
Naomba unielezee vizuri kuhusu hyo reinarnation.
Reply
Defend or die
We acha tu nilipata tabu sana wakati wa kukata roho ni ngumu hiyo afadhali ukate mpingo kwa kiwembe.
Reply
albuluushiy
By Pasco:
Hii ni situation inaitwa "near death experience!" ambayo hutokea kabla ya kifo, wakati ambao roho inaacha mwili!.
Nitawahadithia kidogo experience yang na kuwapa za wengine!.
Niliwahi kupata ajali mbaya sana ya pikipiki, ikasemekana "nimekufa!", nikafunikwa kanga, na kuachwa wakisubiriwa polisi kufika kuuchukua mwili!. Kwa kawaida nikikumbuka huwa napata "stigmata" hivyo subirini nipate kidogo, ndipo nije nihadithie, ilikuwaje hatimaye nikawa hai tena1, na mpaka leo mimi nipo!.
Pasco.
una mambo wewe
Reply
SOURCE: JamiiForums.com